Chama cha Mapinduzi kimewataka wanachama wake visiwani Zanzibar kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tamko
hilo limetolewa huku mazungumzo hakiendelea kutafuta suluhu ya mzozo
kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 ambayo yalifutiliwa mbali.Wito wa wafuasi kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi ume
tolewa baada ya kikao cha kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar katika afisi kuu za chama Kisiwandui.
“Kikao kimewataka wana CCM kujiimarisha, kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kuanzia Rais, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani wakati utakapowadia,” taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo inasema.
Chama hicho hata hivyo kinasema kinaridhishwa na mazungumzo yanayoendelea kuhusu mzozo huo Zanzibar.
“Kikao pia kimeridhia majadiliano yanayoendelea kuhusu hali ya Kisiasa Zanzibar yanayoshirikisha Viongozi kadhaa wakiwemo Marais Wastaafu wa Zanzibar,” taarifa hiyo, iliyotolewa na katibu wa kamati maalum ya halmashauri hiyo Bw Waride Bakari Jabu inaongeza.
Jumamosi, Rais wa Muungano wa Tanzania John Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein.
Akizungumza baada ya mkutano huo, Dkt Shein alisema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumpasha Rais Magufuli juu ya hali ya mazungumzo ya kisiasa Zanzibar.
Mazungumzo hayo yalianza tarehe 9 Novemba na, kwa mujibu wa Dkt Shein, bado yanaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni