Mgawanyiko katika kanisa la
Kianglikana kuhusu suala la mapenzi ya jinsia moja halitakuwa janga bali
itakuwa ni kufeli. Hii ni kwa mujibu wa askofu mkuu wa Canterbury,
Justin Welby.
Akizungumza kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa kanisa hilo Welby, anasema kuwa anataka kuwepo uwiano lakini hiyo ina maana ya kupata njia za kutofautiana kwa nja iliyo nzuri.
Kanisa la kianglikana lina waumini karibu millioni 80 kote duniani katika zaidi ya nchi 160, wengi wakiwa wanamuona askofu Welby kama uongozi wa kanisa hio.
Watunza sera wanasema kuwa kanisa la kianglikana ni lazima lishikilie tamaduni zake.
Lakini maoni ya nchi nyingi za Afrika ambapo mapenzi ya jinsia moja ni makosa, hufanya mambo kuwa magumu kwa kanisa hilo kuwa na msimamo mmoja, huku makanisa mengi yakipinga vikali ndoa za jinsia moja na mskofu shoga.
Kuna wasi wasi kuwa waakilishi kutoka nchi za Afrika huenda wakaondoka kwenye mkutano wa Canterbury.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni