Msemaji wa chama
cha Forum for Democratic Change Ssemujju Ibrahim Nganda amethibitisha
kwamba mgombea urais wa chama hicho Dkt Kizza Besigye amekamatwa.
Amekamatwa akiwa eneo la Naguru, Kampala katika nyumba ambayo upinzani ulidai wizi wa kura ulikuwa ukifanyika.
Wafuasi wa upinzani, Besigye akiwemo, walitaka kukagua nyumba hiyo lakini wakazuiliwa.
Besigye alikamatwa na maafisa wa polisi walioondoka naye kutoka eneo hilo.
Haijabainika amepelekwa wapi.
Hii na mara ya pili kwa Dkt Besigye kukamatwa wiki hii.
Jumatatu, alikamatwa alipokuwa akijaribu kupitia katika barabara moja mjini Kampala.
Polisi walisema hakuwa na idhini ya kupitia eneo hilo kwa mujibu wa sheria.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni