18 Februari 2016

Papa Francis: Donald Trump 'si mkristo'


Papa Francis asema Donald Trump si mkristo
Mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump la kujenga ukuta kati ya Mexico na Marekani si
ukristo.
Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si mkristo
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Trump amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la
Licha ya kuwaambia waumini wa kanisa Katoliki kuwa hatawazuia kutumia uhuru wao kumchagua rais wanaompenda, papa Francis amesema kuwa iwapo Trump anapanga kujega ua basi ''si mkristo''
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwenyenye Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Mtazamo huo wa papa Francis bila shaka unatarajia kuwapa wapinzani wa Trump fataki huku wakiendelea na kura za mchujo ambapo msimamo wa kidini wa mgombea unatazamwa na wapiga kura wengi kuwa kigezo muhimu.
1 kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728