14 Novemba 2015

Watu 127 wauawa katika mashambulio Paris


Ufaransa 
Image caption Manusura wamekuwa wakiondolewa eneo la Bataclan kwa mabasi
Ufaransa imetangaza hali ya hatari na kufunga mipaka yake baada ya watu zaidi ya 127 kuuawa kwenye mashambulio kadha mjini Paris.

Watu 127 wameuawa katika ukumbi wa sanaa wa Bataclan, katikati mwa mji wa Paris.
Watu wenye silaha walishika mateka watu waliokuwa kwenye ukumbi huo kabla yao kuzidiwa nguvu na maafisa wa polisi.
Watu wengine waliuawa kwenye mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa michezo wa taifa wa Stade de France ambako mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani ilikuwa ikiendelea.Uwanja
Image copyright
Image caption Mashabiki waliingia uwanjani baada ya milipuko kutokea Stade de France
Wasimamizi wa mji wa Paris wamewataka raia kusalia manyumbani na wanajeshi 1,500 wametumwa kushika doria Paris.
Shambulio mbaya zaidi linaonekana kuwa hilo la Bataclan, ambako ripoti zinasema watu waliokuwa wamehudhuria tamasha ukumbini walipigwa risasi na kuuawa baada ya kushikwa mateka.
Akiongea baada ya kufika katika ukumbi huo baadaye, Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameapa kuwa wahusika watakabiliwa "bila huruma".
Image copyright AFP
Image caption Rais wa Ufaransa Francois Hollande amehutubia taifa
Mashambulio mengine yalitokea karibu na mighahawa ya Le Petit Cambodge na Le Carillon katika mtaa nambari 10 ambako mwandishi wa BBC anasema aliona watu 10 wakiwa wamelala chini, wakiwa wamejeruhiwa vibaya na wengine kufariki
Mtu aliyeshuhudia ameambia gazeti la Liberation kwamba naye alisikia risasi zaidi ya 100 zikifyatuliwa katika mghahawa wa La Belle Equipe katika mtaa nambari 11.
Milio ya risasi pia ilisikika katika kituo cha kibiashara cha Les Halles.
Rais wa Marekani Barack Obama amelitaja shambulio hilo kuwa "jaribio lisilokubalika la kuhangaisha raia wasio na hatia" na kuahidi kusaidia Ufaransa kukabiliana na waliohusika.
"Hili si shambulio tu dhidi ya raia wa Ufaransa. Ni shambulio dhidi ya binadamu wote na maadili yetu ya pamoja," amesema.
Image copyright
Image caption Hawa ni polisi wa Ufaransa wakiwa karibu na eneo la ukumbi wa Bataclan
"Tutafanya kila tuwezalo kuwasaidia watu wa Ufaransa na mataifa kote duniani kuhakikisha magaidi hawa wanakabiliwa.”
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amesema ameshtushwa sana na shambulio hilo na kuahidi kufanya "lolote tunaloweza kufanya kusaidia."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728