Kundi la wapiganaji la Islamic State
limetoa taarifa kusema kuwa lilifanya mashambulio ya mjini Paris Ijumaa
usiku ambapo watu kama 127 waliuwawa.
Rais Hollande ameelezea
mashambulio hayo kuwa kitendo cha vita vilivotangazwa na IS ambao
alisema walipata msaada kutoka ndani ya nchi. Image copyrightPAImage caption
Shambulizi Paris
Ametangaza hali ya dharura.
Wanaume wanane
waliovaa vizibau vyenye mabomu walikufa kwenye mashambulio hayo katika
sehemu sita mbalimbali za mji mkuu wa Ufaransa. Image copyrightAPImage caption
Usalama waimarishwa Paris
Wakuu wanasema paspoti ya Syria ilionekana karibu na mwili moja.
Watu kama 80 walikufa katika tamasha la muziki wa roki - ambako washambuliaji waliwakabili mateka wao na kuwapiga risasi. Image copyrightEPAImage caption
Maafisa wa polisi waimarisha doria za usalama Paris
Hapo awali, watu waliokuwa na silaha walifyatua risasi nyingi dhidi ya mikahawa iliyo karibu na kusababisha hasara kubwa.
Wengine waliripua mabomu karibu na uwanja wa michezo wa taifa, ambako Ufaransa ikicheza mechi ya kandanda na Ujerumani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni