Mkuu wa kanisa
katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa
chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump la kujenga ukuta
kati ya Mexico na Marekani si
ukristo.Papa Francis alisema kuwa kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta badala ya kujenga daraja huyo si mkristo
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwenyenye Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
1 kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni