Rapa wa Marekani 50 Cent amechapisha picha ya nyumba yake mpya iliyoko barani Afrika katika mitandao wa kijamii ya instragram.
Picha hiyo imezua mjadala hususan baada mwanamuziki huyo nguli wa kizazi cha kufoka, kuwasilisha ombi mahakamani akidai amefilisika.
Katika ujumbe wake huo 50 cent amesema kuwa yu karibu kukamilisha ujenzi wa nyumba yake akiahidi kuandaa dhifa la kukata na shoka kwaajili ya ufunguzi wa jumba hilo.
Mwezi Julai alishtakiwa kwa kosa la kutomlipa dola milioni tano za Marekani $5m mwanamke mmoja ambaye alichapisha kanda yake ya video ya ngono katika mtandao wa intaneti.
Mwimbaji huyo wa muziki wa kufoka hakufafanua ni wapi nyumba yake ilipo lakini amesema anaishi maisha mazuri.
Video hiyo ilionyesha watu wakifanya kazi kando ya nyumba hiyo.
Rapa huyo anayejulikana kama Curtis James Jackson III alisema kuwa alipokuwa akisema amefilisika ilikuwa njia tu ya kujilinda kibiashara.
Yamkini 50 Cent ni mfanyibiashara wa haiba ya juu mwenye hisa na usemi katika makampuni kadhaa yanayoshughulika na mavazi,vinywaji , dondi na uchimbaji madini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni