08 Septemba 2015

Al Shabaab wadai kuteka askari wa Uganda

 
Wapiganaji wa Al Shabaab 
 
Wapiganaji wa kiislamu wa Alshabab wamesema katika maneno yao kuwa linawashikilia mateka wa kivita kutoka Uganda waliowateka wakati wa mashambulizi ya wiki iliyopita.

Uganda imesema kuwa wanajeshi kumi na mbili waliokuwa chini ya jeshi la umoja wa Afrika wakilinda amani nchini Somalia waliuawa katika shambulio hilo kwenye ngome yao iliyopo kusini mwa nchi hiyo.
Wanadiplomasia wa nchi za magharibi wamesema kuwa zaidi ya wanajeshi mia moja wa Uganda aidha wamekufa au hawajulikani walipo.
Afisa mmoja wa kundi la Alshabab amesema wanajeshi hao wa Uganda wapo salama na wana afya njema.
Hakuweza kusema ni wangapi walioshilikiliwa ama nini kinaweza kutokea kwa mateka hao.
Amesema Uganda imefanya makosa ilipotamka juma lililopita kuwa wanajeshi wake wote wamehesabiwa.
Katika siku kadhaa zilizopita wanamgambo hao wa Al Shabaab walitumia picha za askari waliofariki wa Umoja wa Afrika na vifaa vyao katika kuendeleza propaganda zao.
Ingawa kundi hilo hivi karibuni limepoteza maeneo mengi nchini Somalia, juma lililopita lilikamata miji miwili iliyokuwa iliyoachwa na jeshi la umoja wa Afrika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728