Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA)
limeshutumiwa mtandaoni kwa kusimulia moja kwa moja matukio
yaliyopelekea kuuawa kwa Osama Bin Laden.
Shirika hilo limekuwa likiandika ujumbe kwenye Twitter na kusimulia matukio yaliyopelekea kuuawa kwa kiongozi huyo wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda kana kwamba yalikuwa yanafanyika leo.
Siku ya leo ni miaka mitano tangu kuuawa kwa Osama Mei 2011 katika nyumba moja mjini Abbottabad, Pakistan.
Alikuwa amesakwa na Marekani na washirika wake kwa mwongo mmoja.
CIA wamekuwa wakitoa maelezo kuhusu mipango na ukusanyaji wa habari za kijasusi ambazo zilipelekea Osama kuuawa.
Mmoja wa watu katika Twitter ameandika kwamba hatua hiyo ni ya “kujiaibisha”. Wengine wametumia vibonzo na picha wakitumia mikono yao kufunika macho yao wasione.
Bw Osama alituhumiwa kuamrisha kutekelezwa kwa mashambulio ya 9/11 mjini New York na Washington.
Mkurugenzi wa CIA John Brennan amesema ilikuwa muhimu sana kumwangamiza Bw Osama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni