Wakuu wa Jamhuri ya Demokrasi ya
Congo wanasema wamemkamata naibu kamanda wa
kundi la wapiganaji,
linalohusishwa na mauaji makubwa ya Rwanda ya mwaka 1994.Msemaji wa serikali, alieleza kuwa Jenerali Leopold Mujyambere, wa kundi la Rwanda la FDLR, alikamatwa mjini Goma, mashariki mwa nchi.
Kundi la FDLR ni la Wahutu wanaoshutumiwa kuuwa malaki ya Watutsi na Wahutu waliokuwa na msimamo wa wastani, wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Rwanda imeingilia kati kijeshi mashariki mwa Congo katika juhudi za kuliangamiza kundi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni