07 Mei 2016

Dini hudhuru wanafunzi, wizara ya elimu China yasema

DiniSerikali katika mkoa wa Gansu, China imeagiza wasimamizi wa shule kutekeleza kikamilifu marufuku ya kutokubalia shughuli zozote za kidini shuleni.

Wizara ya elimu katika mkoa huo uliopo kaskazini mashariki kwa nchi hiyo imechukua hatua hiyo baada ya msichana mmoja kuoneshwa kwenye video akikariri vifungu kadha vya Koran katika shule moja.
Shule hiyo imeshutumiwa vikali na maafisa hao wa wizara ya elimu.
Wizara hiyo kupitia taarifa imesema dini shuleni huathiri hali ya kiakili ya watoto.
Baadhi ya shughuli za kidini hukubaliwa nchini China lakini hudhibitiwa vikali.
Lakini waandishi wa BBC nchini humo wanasema serikali huwa makini sana kuhusu baadhi ya shughuli za kidini ambazo zinaweza kuathiri utambulisho wa kitamaduni wa Kichina.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728