
Leo imetimia miaka mitatu tangu aliekuwa staa nguli wa Bongo
Movies, Steven Kanumba afariki dunia, hizi ni baadhi ya jumbe ambazo
mastaa kutoka Bongo Movies wameziandika kuonyesha kumbukumbu zao kwa
staa huyo.
Ni siku ambayo siwezi kusahau maisha yangu yote pumzika kwa amani
kanumba wangu., nilikupenda ila mungu alikupenda zaidi . Pumzika kwa
amani.
Johari
Huwezi kutaja mafanikio ya bongo movies bila kukutaja wewe...tunakuthamini na tunakukumbuka milele
JB
Steven Charles Kanumba pengo lako mpaka leo atujaweza kuliziba na
sidhani kama tutaweza tena ingawa Sasa umetimiza miaka mitatu tangu
ulipotuacha ghafla kiukweli ni ngumu sana kusahau Tutakukumbuka daima
kwani tunapozungumzia kiwanda cha sinema nchini lazima tulitaje jina
lako kaka angu ...R.I.P KANUMBA.