Bosi wa Manchester City Manuel Pellegrini anaamini watambakisha kiungo Frank Lampard.
Kiungo huyo mwenye miaka 36 yuko Manchester City kwa mkopo akitokea New York City,lakini Man City wanataka kumbakisha klabuni hapo kwa muda mrefu.
"Frank ni mchezaji muhimu kwa timu natumaini ataendelea kuwepo hapa," alieleza Pellegrini.
Lampard amekua mchezaji muhimu akiwa amefunga magoli 6 katika mechi 15 aliyocheza na anaoneka atakua mbadala wa Yaya Toure ambae ataenda kuliwakilisha taifa lake katika michuano ya kombe la Afrika mwezi Januari.
Man City wanataka kumalizana na Lampard kabla ya timu yke inayomliki hawajaanza na maandalizi ya msimu mpya wa ligi ya Marekani .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni