SUPASTAA, Cristiano Ronaldo Jumamosi iliyopita alipiga ‘hat-trick’ yake ya 23 kwenye La Liga na kuweka rekodi wakati alipoiongoza Real Madrid kuichapa Celta Vigo mabao 3-0.
Wakati Ronaldo akitamba kuweka rekodi hiyo, mpinzani wake wa karibuni Lionel Messi juzi Jumapili alijibu baada ya kufunga ‘hat-trick’ na kufikisha zaidi ya mabao 400 katika Klabu ya Barcelona wakati walipoichapa Espanyol mabao 5-1 kwenye La Liga.
Messi, anayeshikilia rekodi ya mabao kwenye La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya aliendeleza makali yake ya kupiga mabao na kufikisha idadi ya mabao 402 kwenye kikosi cha Barca, yakiwamo mabao 28 kwenye mechi za kirafiki.
Messi sasa amezidiwa ‘hart-trick’ mbili na Ronaldo kwenye La Liga, lakini staa huyo Muargentina amefunga jumla ya hat-trick 27 dhidi ya 27 za Ronaldo kwenye mechi zote walizochezea klabu hizo za Hispania.
Kasi hiyo ya ufungaji wa mabao wa mastaa hao inachochea vita ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia ambao mastaa wote hao wawili wametinga hatua ya fainali sambamba na kipa wa Ujerumani na Bayern Munich, Manuel Neuer
14 Desemba 2014
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni