Wapiganaji wa Al shabaab wamefanya shambulizi katika kambi kuu ya jeshi la Umoija wa Afrika karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu Somali.
Milipuko na milio ya risasi ilisikika ndani ya kambi hiyo kulingana na kanali Ali Houmed aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
Alshabaab imekiri kutekeleza shambulizi hilo na kwamba wapiganaji wake wako ndani ya kambi hiyo.
Jeshi la African Union lina zaidi ya wanajeshi 20,000 nchini humo ili kuisadia serikali ya Somali kukabiliana na Al-shabaab.
Sheikh Abdiasis Abu Musab,ambaye ni msemaji wa kundi la Alshabaab amesema kuwa wapiganaji wa kundi hilo waliingia kwa nguvu ndani ya kambi hiyo.
Wapiganaji wetu wameingia katika kambi hiyo ya Halane kwa nguvu kupitia lango kuu na sasa mapigano yanaendelea ndani ya kambi hiyo.
Kambi hiyo ya jeshi iko karibu na uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Kambi hiyo pia ni makao ya balozi za Uingereza na Italy na hutumiwa kama makao makuu ya operesheni za umoja wa mataifa nchini Somali.
Aleem saddique ,ambaye ni msemaji wa umoja wa mataifa nchini somali ameikiambia chombo cha habari cha Reuters kwamba wafanyikazi wote wa umoja wa mataifa wako salama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni