HALI ya tafrani ilizuka jijini Dar es Salaam jana, baina ya Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa na
askari wa Jeshi la Polisi.
Hali hiyo ilijitokeza, baada ya askari polisi kumhoji kiongozi huyo wa
chama kikuu cha upinzani nchini, hatua yake ya kufanya mkutano bila
kibali.
Tafrani hiyo ambayo iliibuka katika eneo la Tegeta Gereji ilianza saa
11:50 jioni baada ya Dk. Slaa kuwasili katika eneo hilo na kuanza
kuhutubia ambapo wananchi walitoa malalamiko yao dhidi ya Mkuu wa Wilaya
ya Kinondoni, Jordani Rugimbana kwa kumilikisha eneo hilo kwa
mwekezaji.
Akizungumza baada ya wananchi kuwasilisha malalamiko yao, Dk. Slaa
alisema kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakitenganishwa na vyama ila
linapojitokeza suala lenye maslahi kwa Taifa huwa wanaondoa itikadi zao.
“Haiwezekani Serikali iwakabidhi eneo alafu leo iwaondoe ni jambo ambalo
halikubaliki kwani mwekezaji mmoja hawezi kuwa na manufaa kushinda watu
4000.
“… lakini pia biashara ya magari inahitaji sehemu kuliko na magari sasa
wakiwahamisha hapa na kuwapeleka huko wanakosema kazi zenu mtafanyaje
inatakiwa mshikamane kwenye hili mwache woga.
“Mimi nitawasaidia mkionyesha jitihada kwani nalipwa ruzuku kutokana na
kodi zenu hivyo nipotayari kuwapigania hivyo jumatatu nitatoa mawakili
kwa ajili ya kupitia agizo hili kwani huwezi kumwacha mwananchi
anaondolewa kwenye eneo hili naomba sasa mtambue kuwa kama ni ukombozi
sasa umeanza,” alisema Dk Slaa.
Ilipotimu saa 11:40 jioni polisi walivamia eneo hilo, ambapo aaskari
mmoja alkwenda katika jukwaa alilokuwa akihutubia Dk. Slaa na kutaka
kumkamata hali iliyozusha malumbano makali kati ya wananchi na polisi
Dk Slaa alihoji kwa kusema: “Wewe ni nani, unataka nini na unatoka wapi?
Polisi: Mimi natoka ofisi ya juu, ni nani aliyekupa kibali cha kufanya
mkutano hapa?,” alihoji askari.
Kutokana na hoja hiyo Dk Slaa alijibu: “Kwani Kikwete anapofanya mkutano
huwa anapewa kibali na nani?, si akijisikia tu anafanya?,” alihoji Dk.
Slaa.
Mara baada ya majibizano hayo, wananchi waliokuwa wamekusanyika katika
eneo hilo walianza kuzomea huku wakiwatuhumu askari polisi kuwa ndio
imekuwa mazoea kwao kukamata watu.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyeviti wa Serikali za Mitaa yote sita ya Kata Kunduchi wa CCM pamoja na wale wa Chadema.
MTANZANIA ilimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ili
kuweza kupata ufafanuzi kuhusu madai hayo, ambapo alisema hawezi
kuzungumzia suala hilo kwani kilichofanyika ni kusimamia agizo la
mahakama.
30 Desemba 2014
Dk. Slaa, polisi wapambana Dar
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni