Uongozi wa Timu ya Manchester United umesema upo tayari kutoa paundi milioni 120 kwaajili ya kumsajili winga Gareth Balle mwenye umri wa miaka 25 kwa mwezi januari kutoka klabu ya Real Madrid , winga ambaye ni miongoni mwa wachezaji ghali zaidi ulimwenguni.
Gareth Bale alijiunga na Real Madrid kwa kuweka rekodi kubwa duniani kwa usajili wa rekodi ya paundi milioni 85.3 mwaka 2013.
Wakati huo huo kocha Laurent Blanc wa Timu ya Paris St Germain anafikiria kumsajili mshambuliaji Edinson Cavani( 27), kwa gharama ya pauni milioni 50 ikiwa ndio hitaji la Timu ya Arsenal katika katika usajili wa mwezi Januari 2015.
Nayo klabu ya Manchester City inandaa pauni milioni 25 katika jitihada za kutaka kumsajili msahambuliaji wa Atletico Madrid Mario Mandzukic (28).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni