Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, kamanda wa polisi wa Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alisema mauaji hayo yalitokea juzi saa 8:00 usiku katika Kijiji cha Kireguru, Kata ya Kwediboma wilayani Kilindi wakati hao walipovamia nyumba ya dereva huyo.
Alisema uchunguzi umebaini kuwa dereva huyo alikuwa na ugomvi wa muda mrefu na mtu mmoja, ambaye kamanda hakumtaja jina lake, akimtuhumu kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mkewe.
“Uchunguzi wetu wa kipolisi umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mambo ya mapenzi, alikuwa na uhusiano na bibi wa watu na aliwahi kukanywa aache tabia hiyo akakaidi,” alisema Kashai.
“Ila kitendo kilichofanyika ni cha kikatili na hakikubaliki. Tunaendelea na uchunguzi kubaini watu waliohusika ili tuwafikishe katika vyombo vya sheria.”
Katika tukio jingine, kamanda huyo alisema polisi wanawashikilia watu wanne wakazi wa wilayani Handeni kwa tuhuma za kumuua kwa kumnyonga hadi kufa mwanafunzi wa darasa la sita wa Shule ya Msingi ya Kivesa, Isaka Beda na mwili wake kuutundika juu ya mti.
Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 10:00 jioni eneo la Chanika baada ya watu waliokuwa wakienda shambani walipouona mwili wa marehemu ukining’inia juu ya mti.
Alitoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na kuahidi kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua kama wahalifu wengine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni