Bunge la Somalia limeidhinisha uteuzi wa waziri mkuu mpya akiwa ni afisa wa tatu kuhudumu katika wadhfa huo katika kipindi cha miaka miwili.
Wengi wa wabunge walimpigia kura Omar Ali Sharmarke.
Mapema mwezi huu walipitisha mswada wa kutokuwa na imani dhidi ya aliyekuwa waziri mkuu Abdiweli Sheikh Ahmed,baada ya majaribio matatu ya kutaka kumuondoa madarakani kuambuliwa patupu.
Waandishi wanasema kuwa serikali ililemazwa na vita villivyokuwa kati ya wafuasi wa Abdiweli dhidi ya wale wanaoumuunga mkono rais Hassan Sheikh Mohamud.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni