14 Desemba 2014

Aguero nje kwa mwezi mmoja

NI sawasawa na Barcelona kucheza bila ya Lionel Messi au Real Madrid kucheza bila ya Ronaldo. Manchester City wanatazamiwa kuwa na kibarua kigumu baada ya habari kuwa staa wao, Sergio Aguero atakuwa nje kwa mwezi mzima.


Aguero aliumia goti katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton Jumamosi jioni na amewaambia rafiki zake kwamba atakuwa nje kwa mwezi mzima huku akikosa mechi muhimu za Man City hasa kipindi cha Sikukuu ya Krismasi.

Kwa kuanzia, Aguero atalikosa pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya AS Roma ambalo linaamua hatima yao kama wataweza kuingia katika hatua ya 16 bora itakayopigwa Februari mwakani.

Kuna wasiwasi pia Aguero atakosa mechi tano za Ligi Kuu ya England dhidi ya Leicester City, Crystal Palace, West Brom, Burnley na Sunderland. Aguero pia anaweza kulikosa pambano la kwanza la Man City na michuano ya FA Januari mwakani.

Juzi Man City walikuwa tayari kumruhusu Aguero kusikilizia maumivu ya goti lake kwa saa 48 zaidi kabla ya kwenda katika vipimo. Ni vipimo hivyo ndivyo ambavyo vinaweza kutoa jibu sahihi Aguero atakuwa nje kwa muda gani lakini mwenyewe ameelezea hofu yake ya kuwa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja huku akidai kwamba ‘alisikia maumivu makali alipoumia.’

Kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini, hata hivyo amekataa kukubali madai yanayotolewa na wachambuzi wa masuala ya soka kwamba timu yao imekuwa ikimtegemea zaidi Aguero pekee ambaye mpaka sasa ameshafunga mabao 19 msimu huu.

“Tungependa kucheza na Sergio lakini sidhani kwamba anatubeba peke yake. Nadhani Ronaldo ni muhimu sana kwa Real Madrid na Messi ni muhimu sana kwa Barcelona lakini sidhani kama timu hizo zinabebwa na mchezaji mmoja,” alisema kocha huyo raia wa Chile.

Kwa msimu huu, Man City imejikuta katika wakati mgumu kutokana na kuathiriwa na tatizo la majeruhi mara kwa mara hasa kwa wachezaji wake tegemeo. Kiungo David Silva anatazamiwa kukipiga katika pambano la kesho dhidi ya Roma akiwa ndiyo kwanza anarudi kutoka katika majeraha.

Mwingine ni nahodha Vincent Kompany ambaye anatazamiwa kucheza katika pambano hilo dhidi ya Roma ingawa amekuwa akiathiriwa na majeraha siku za hivi karibuni

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728