22 Desemba 2014

Jaji Warioba apigwa vita

Mwanza. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba amesema licha ya kushambuliwa kwa mambo ya msingi anayozungumza kuhusu Katiba Mpya hakuna mtu aliyejitokeza kumjibu hoja zake, zaidi kumpiga vita kwa kutumia njia wanazo jua.

Pia, Jaji Warioba alisema watu hao wanaomshambulia wamekuwa wakitoa majibu mepesi kwamba yeye amemsaliti Mwalimu Julius Nyerere lakini kwa mambo anayoyazungumza hata Mwalimu Nyerere akija leo atamuunga mkono.
Wakati Jaji Warioba akisema hayo jana kwenye mdahalo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Joseph Butiku alisema kamwe mtu huwezi kutengeneza Katiba kama ni muongo, mnafiki na mtu unayethamini tumbo lako na familia yako.
Akizungumza kwenye mdahalo huyo uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest mkoani hapa na kuhudhuliwa na mamia ya watu, Jaji Warioba alisema kama tunataka kupata kitu kizuri hatuwezi kukipata kwa kutumia lugha za matusi wala kejeli.
Jaji Warioba alisema, “Mimi nimekuwa nikizungumza mambo ya msingi kuhusu Katiba Iliyopendekezwa, lakini hakuna anayejitokeza na kunijibu, zaidi ya kunijibu kwa mambo mengine wanayoyajua wao.”
Aliongeza, “Katika majibu yao makubwa utawasikia wanasema mimi nimemsaliti Mwalimu Nyerere, kuna baadhi ya mambo ninayoyasema hata Mwalimu Nyerere angekuja leo angeniunga mkono.”
Warioba alisema wao walipendekeza mambo mengi kuhusu maadili kwenye Katiba Iliyopendekezwa, lakini Bunge Maalumu la Katiba liliyaondoa na kubakiza mamchache, huku wakieleza kwamba mengine yatatungiwa sheria.Alisema sheria wakati wowote viongozi wanapotaka wanaweza kuibadilisha, lakini Katiba siyo rahisi kuibadilisha ndiyo maana Tume ikapendekeza mambo mengi kuhusu maadili ya viongozi.
“Tumekuwa mastari wa mbele kupigania usuala la maadili ya viongozi yawemo kwenye Katiba, suala la maadili hata Mwalimu Nyerere alikuwa akilitilia makazo, kwani mfano hai aliuonyesha mwaka 1984 pale alipoongoza mjadala wa CCM kuwa na ukomo wa urais.
Alifanya hivyo na yeye akiwa Rais sasa mimi nitamsaliti vipi, wakati sauala la maadili alikuwa akilipigania hata yeye,” alisema Jaji Warioba.
Warioba alisema mbali na hilo Mwalimu  Nyerere aliwahi kupitisha ajenda kwamba Wabunge wakae kwenye majimbo yao, Je, angeurudi  leo na wananchi wakamueleza  jinsi hali ilivyo tunazani angekubaliana na jambo hilo, hivyo kwa taifa lolote maadili ya viongozi ni kitu cha msingi.
Jaji Warioba alisema jukumu lilipewa Tume ya uchaguzi ambayo itasimamia kura ya maoni ni kubwa na kwamba muda uliyipo ni mdogo na wananchi wanatakiwa kupewa elimu ya kutosha.
“Kura ya maoni kwa Katiba iliyopendekezwa itafanyika mwakani mwezi Aprili, huku kampeni zikitarajia kuanza mwishoni mwa mwezi Machi, kwa kweli kuna kazi kubwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa jukumu la kusimamia kura hiyo, lakini ni vyema wananchi wakapewa elimu ya kutosha,” alisema.
Butiku
Akizungumza kwenye mdahalo huo Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku alisema wao wanafanya kazi ya kuwaelewesha wananchi nini maana ya Katiba, kwani Katiba ni sheria mama kwenye nchi ya watu wastarabu.
“Huwezi kutengeneza Katiba kama wewe ni muoga, mnafiki unayetaka Kutengeneza Katiba kwa ajili ya tumbo lako. Naomba wananchi elimu hii tunayowapa isiishie hapa mkitoka kwenye mdahalo huu huko mitaani vijiweni nendeni mkazungumze,”alisema Butiku.
Alisema wao washawishi wananchi wakatae Katiba iliyopendekezwa bali wanatakiwa kuismona kwa makini na kuielwa ili ikirudi tena kwao waweze kuchukua maamuzi sahihi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728