Pigano la marudio kati ya Tyson Fury
na Wladmir Klitschko litaandaliwa mjini Manchester mnamo mwezi Julai
tarehe 9 kulingana na mkufunzi wa bondia huyo wa Uingereza.
Peter Fury alituma ujumbe katika mtandao wa Twitter siku ya Ijumaa na tanagazo jingine linatarajiwa baadaye.
Fury ambaye ni mzaliwa wa mjini Manchester na ambaye ana umri wa miaka 27,alimshinda raia wa Ukraine Klitschko kwa pointi mjini Dusseldorf mwezi Novemba ili kushinda mikanda mitatu ya WBA,IBF na WBO.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Fury ni Muingereza wa tano kushinda mataji hayo ya uzani mzito zaidi duniani.
Hatahivyo Fury alipokonywa ukanda wa IBF wiki mbili baada ya ushindi huo na marudiano na Klitschko yanamaanisha kwamba hatokabiliana na bingwa wa uzani huo Vyacheslav Glazkov.
Taji hilo litakuwa wazi siku ya Jumamosi ambapo mshindi wa medali ya dhahabu katika shindano la Olimpiki Anthony Joshua atakabiliana na bingwa mtetezi Charles Martin katika ukumbi wa 02 mjini London.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni