Jeshi la Syria limegundua kaburi
lenye mabaki ya miili kama 40 katika mji wa Palmyra, ambao ulikombolewa
kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State, awali juma hili.
Kati ya mabaki hayo, kulikuwa na miili ya wanawake na watoto, na baadhi ya miili inaonyesha watu walikatwa vichwa.
Palmyra ilikuwa mikononi mwa IS kwa karibu mwaka mzima, na wakati huo, wapiganaji hao waliuwa watu wengi.
Kati yao ni wanaume 25 waliouwawa katika uwanja maalumu uliojengwa zama za Wa-rumi katika mji huo wa kale.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni