Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Amber Rayne amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles ,maafisa wamethibitisha.
Marafiki na waliokuwa wafanyikazi wenzake walituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wakimuenzi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alifariki usingizi wikendi iliopita.
Amber alikuwa nyota wa filamu za ngono kwa muongo mmoja kabla ya kujiuzulu mwaka 2015.
Alikuwa miongoni ,mwa kundi moja la wanawake ambao walidai kwamba James Deen,ambaye pia ni nyota wa filamu za ngono alimshambulia.
Hatahivyo Deen amekana madai hayo.
Mkaguzi wa matibabu katika kaunti ya Los Angeles ameiambia Newsbeat kwamba hakuna sababu rasmi ya kifo chake iliothibitishwa.
Hatahivyo wamesema kuwa familia yake imearifiwa.Bi Rayne ,ambaye jina lake rasmi ni Meghan Wren,alitangaza kujiuzlu kutoka kazi hiyo mwaka uliopita.
Wafanyikazi wenza katika soko la filamu za ngono walituma ujumbe wa kushtushwa na kifo chake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni