Mamba mkubwa mla ng’ombe ameuawa katika jimbo la Florida nchini Marekani.
Mnyama huyo alikuwa na uzani wa kilo 360.Mwindaji Lee Lightsey amesema mamba huyo wa ukubwa wa futi 15 (4.5m) ndiye mkubwa zaidi ambaye amekumbana naye katika kipindi cha miaka 18.
Baada ya kumuua, alihitaji trekta kumbeba.
Bw Lightsey alimgundua mnyama huyo akiwa na mwelekezi wa wawindaji Blake Godwin walipokuwa katika maeneo ya kumnyweshea mifugo maji Jumamosi.
Walimfyatulia risasi mamba huyo alipokuwa umbali wa mita sita kutoka kwao.
"Ingawa mnyama huyu ni mnene hivi, sijashangaa kwamba amekuwepo,” amesema Bw Lightsey.
- Je wajua siri ya Mamba usingizini?
- Mamba kulinda wafungwa hatari Indonesia
- Kwa Picha: Ndovu dhidi ya mamba
"Kilichotuvutia ni kwamba anaonekana amekuwa akiwala ng’ombe wetu, kwa sababu tulipata vipande vya nyama majini. Alikuwa dubwana lililostahili kuangamizwa.”
Bw Lightsey anasema mamba mkubwa zaidi ambaye amewahi kumuua alikuwa na urefu wa futi 13ft (4m).
Mamba wa Marekani hupatikana mashariki mwa Marekani katika majimbo ya Florida na Louisiana, kila jimbo likiwa na zaidi ya mamba milioni moja.
Eneo la kusini mwa Florida ndilo pekee ambalo mamba wa Marekani na mamba wa kawaida huishi kwa pamoja.
Bw Lightsey amesema anapanga kumhifadhi mamba huyo lakini nyama yake ataikabidhi kwa wahisani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni