Burundi imesafirisha mwili wa aliyekuwa waziri wa Rwanda kufuatia kifo chake cha ghafla akiwa kizuizini juma lililopita.
Waziri huyo wa zamani bwana Jacques Bihozagara alikamtwa takriban miezi 4 iliyopita na maafisa wa intelijensia wa Burundi kwa tuhuma kuwa alikuwa ni jasusi wa Rwanda.
Kilichosababisha kifo chake hakijabainika hadi kufikia sasa.
Jamaa wa marehemu bw Bihozagara wanataka mwili wake ufanyiwe uchunguzi wa kina ilikubaini chanzo cha kifo chake.
Serikali ya Rwanda imeitaka Burundi ielezee sababu za kukamatwa kwake na chanzo cha kifo chake.
Rwanda inasisitiza kuwa hakuwa jasusi wake na inasema bwana Bihozagara alikamatwa kinyume cha sheria.
Bw Bihozagara aliwahihudumu kama balozi wa Rwanda kabla ya kuteuliwa kama waziri wa maswala ya vijana nchini Rwanda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni