01 Februari 2015

Profesa Muhongo amuasa Simbachawene kuwa makini

Dar es Salaam. Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo amekabidhi ofisi kwa Waziri wa sasa, George Simbachawene katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake na kumwambia awe makini katika utendaji kazi hasa kwenye mikataba.
Akikabidhi ofisi, Profesa Muhongo alionya kuhusu matumizi mabaya ya Ofisi yanayoambata na rushwa ili kuwasaidia Watanzania masikini wanaoitegemea sekta hiyo kwa maendeleo ya uchumi wao.
Profesa Muhongo amemuasa Simbachawene kuhusu umakini na kufanya kazi kwa kuzingatia mikataba inayoweza kuwanuifaisha Watanzania na rasilimali zao. Simbachawene atasimamia ofisi hiyo kwa miezi sita kabla ya kuvunjwa kwa bunge baadaye Julai.
Hata hivyo, Profesa Muhongo alimsifu Simbachawene kuwa hakuwahi kuonyesha ubinafsi wala tamaa na muda wote alikuwa akizungumzia kuhusu kuwatumikia Watanzania alipokuwa Naibu Waziri wa wizara hiyo, kwahiyo ana imani naye.
Alisema Tanzania ni lazima ilenge katika kujenga uchumi imara kupitia sekta ya nishati na madini inayokua kwa kasi ili Watanzania pia wakue kiuchumi.
Kwa upande wake, Simbachawene alisema ataendeleza mazuri yaliyoachwa na mtangulizi wake kwa kuweka uwazi kwa kila kitu kinachofanyika, kwani ofisi ya umma si mali ya mtu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728