22 Februari 2017

Mourinho: Wayne Rooney anaweza kuondoka Manchester United

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema bado inawezekana Wayne Rooney aihame klabu hiyo mwezi huu.
Mshambuliaji huyo wa
England mwenye umri wa miaka 31 alifunga bao lake la 250 United mwezi uliopita na kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi katika historia ya klabu hiyo.
Hata hivyo, kumekuwa na uvumi kwamba huenda akahamia China.
Soko la kuhama kwa wachezaji Ligi Kuu ya China litafungwa wiki ijayo.
Mourinho aliulizwa iwapo nahodha huyo wa United atakuwa Old Trafford kufikia wakati huo.
"Itabidi mumwulize mwenyewe," Mourinho alisema.
Rooney asawazisha mabao na Bobby Charlton
Rooney kustaafu soka ya kimataifa 2018
"Bila shaka siwezi kuwahakikishia (kwamba atakuwa hapa). Siwezi kuwahakikishia kwamba nitakuwa hapa wiki ijayo, nitawezaje kuwahakikishia kwamba mchezaji atakuwa hapa msimu ujao?"
Mkataba wa Rooney United ni wa hadi 2019 na majuzi alikuwa amedokeza kwamba kuna uwezekano huenda asimalize muda wote huo United.
Amekuwa hapewi nafasi ya kuwa katika kikosi cha kuanza mechi msimu huu na amefunga mabao matano pekee.
Hata hivyo, Mourinho alisema Oktoba kwamba Rooney hakuwa anenda "popote" na alisisitiza Jumanne kwamba hataki mchezaji huyo aihame Manchester United.
"Siwezi kumsukuma - au kujaribu kumsukuma - nyota wa klabu hii ahame," aliongeza Mourinho.
"Hivyo, itabidi mumwulize iwapo anaona kama atakuwa katika klabu hii kipindi kilichosalia cha uchezaji wake au iwapo anadhani atahama.
"Si swali langu hilo kwa sababu ninafurahia kuwa naye. Sitaki aondoke."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728