16 Machi 2017

Jaji mwingine azuia marufuku mpya ya Trump kuingia Marekani

Jaji wa Hawaii amezuia marufuku mpya ya kuingia Marekani iliyowekwa na Rais Donald Trump, saa chache kabla ya
kutakiwa kuanza kufanya kazi, Alhamis hii.

Jaji Derrick Watson amesema kuna ushahidi wenye uwalakini kuhusu madai ya serikali kuwa marufuku hiyo ni kwaajili ya usalama wa nchi.

Amri hiyo ingefanya kuwepo marufuku ya siku 90 kwa raia kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani na siku 120 za kuzuia wakimbizi.

Trump anasisitiza kuwa hatua hiyo ni kwaajili ya kuzuia magaidi kuingia nchini Marekani lakini wakosoaji wanaielezea kama ya kibaguzi. Awali, marufuku hiyo ilipingwa na jaji wa Seattle.

Akizungumza kwenye mkutano huko Nashville, Tennessee, Jumatano jioni, Trump alisema hatua hiyo ya jaji wa Hawaii inaifanya Marekani ionekane dhaifu.

Alisema ataendelea kuipigania na kwamba ,”We’re going to win.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728