02 Novemba 2014

USAFIRI DAR NI HATARI

Dar es Salaam. Maisha ya maelfu ya Watanzania yapo hatarini baada ya kubainika kuwa kwenye magari ya abiria maarufu daladala ya jijini humo, yanayotoa huduma za usiku kwa safari za kwenda na kutoka maeneo mbalimbali yamekuwa yakihusishwa na mtandao wa vibaka unaoendesha vitendo vya uporaji na ukabaji.

Mtandao huo unaelezwa kufanya vitendo hivyo kwa kutumia silaha mbalimbali ikiwamo visu na bastola, huku baadhi ya vibaka hao wakitumia magari hayo kujificha kwa kujifanya ni abiria.
Mbali na uhalifu huo unaoendelea kufanyika kwenye daladala nyakati hizo za usiku, magari mengi yanayotoa huduma za usafiri nyakati hizo hadi alfajiri ni mabovu yakiwa pia hayana vibali vya kutoa huduma hizo.
Magari hayo yanayofahamika kwa jina la ‘daladala bubu’ au ‘ya kuwanga’ madereva wake pia hufanya kazi hiyo bila ya kuwa na leseni za udereva, jambo linalohatarisha zaidi maisha ya abiria.
Uchunguzi wa gazeti hili katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo ikiwamo Sinza, Ubungo, Kariakoo, Faya, Buguruni, Gongo la Mboto Machinjioni, Kimara, Mbezi, Magomeni, Kinondoni, Tandika, Temeke, Yombo Dovya, Vingunguti, Bom Bom na Machimbo, umebaini kuwa magari hayo hufanya kazi nyakati za usiku pekee kutokana na kutokuwapo askari ama kuwapo askari wachache wa Kikosi cha Usalama Barabarani.
Gazeti hili limebaini kuwa wizi kwenye daladala hizo, madereva wa daladala kuwapa makondakta au wapiga debe kuendesha magari ya abiria vinaendelea kushamiri, huku nyakati za hatari zaidi kwa daladala hizo ni kuanzia saa 6 usiku hadi alfajiri.
Uhalifu unaofanywa
Uhalifu unaofanywa kwenye magari hayo unahusisha vibaka wanaokuwa ndani ya gari ambao hujifanya kuwa miongoni mwa abiria.
Imebainika kuwa abiria akikaa vibaya ndani ya daladala, vibaka hao hutumia nafasi hiyo na kujihalalishia chochote watakachoweza kuibia.
Aina nyingine ya vibaka ni wale wanaokula njama na madereva na kondakta wa daladala. Vibaka hao pia hujifanya abiria kwenye daladala bubu husika ambapo wakifika kituoni hujihusisha na kupiga debe kuita abiria, lakini mbele ya safari dereva hubadili njia, akiweza kwenda vichochoroni ndipo abiria huvamiwa na kuporwa mali zao huku wakitishiwa kwa silaha.
Uchunguzi unaonyesha kuwa aina nyingine ya wizi huo hufanywa na kundi la vibaka ambalo hujifanya ni abiria ambapo kila mmoja hulenga kumfanyia uhalifu abiria mmoja.
“Abiria akishuka tu na yeye anashuka, humfuata na kumwibia, halafu anakwambia utembee bila kugeuka. Ukigeuka tu wanakuchoma na kisu au silaha yoyote wanayokuwa wamejihami nayo,” alieleza mmoja wa madereva wa daladala aliyeomba jina lihifadhiwe kwa kuwaogopa vibaka hao.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728