19 Novemba 2014

Watendaji waliohujumu fedha kukiona

 Mufindi. Watumishi wa Wilaya ya Mufindi wanaotuhumiwa kutafuna fedha za halmashauri hiyo, watajulikana Novemba 24 mwaka huu baada ya kufanyika kwa kikao cha kamati ya fedha.
Sakata hilo lilianza mwishoni mwa wiki baada ya baraza la madiwani la halmashauri kuibua ufisadi wa Sh291.7 milioni zinazodaiwa kulipwa kwa kampuni za ukandarasi kwa ajili ya kazi ya nyongeza iliyotolewa na watendaji kinyume na Sheria ya Ununuzi namba 40 (1) ya mwaka 2005.
Mwenyekiti wa halmashauri, Peter Tweve alisema kuwa wahusika wote watachukuliwa hatua za kisheria bila kujali nafasi zao.
Tweve alisema katika kazi hizo zilizoongezwa bila kufuata taratibu, watumishi hao walifanikiwa kujichotea Sh2.7 milioni.
“Tunamshukuru sana mkaguzi wetu wa ndani kwa kazi nzuri aliyoifanya. Baada ya kubaini matumizi hayo mabaya ya fedha, baraza limeiagiza ofisi ya mkurugenzi kuwabaini wote waliohusika na kuwachukulia hatua za kinidhamu kabla mamlaka nyingine hazijachukua hatua,” alisema Tweve.
“Katika hili, tunamtaka yeyote aliyehusika awe mkurugenzi mtendaji au mwekahazina awajibike... tunachotaka wote wachukuliwe hatua kali ili iwe fundisho kwa watakaobaki,” alisema.
Pia alisema kwa sasa kuna kazi zinazoendelea katika sekta ya ujenzi ambazo zilifuata taratibu.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri, Athuman Kihamia alisema ofisi yake imepokea maelekezo ya kiutendaji kutoka kwa madiwani, hivyo watahakikisha wanayafanyia kazi, ili kazi zikamilike kwa wakati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728