02 Mei 2016

Binti wa Obama, Malia kusomea Harvard

Mwanaye rais wa Marekani Barack Obama, Malia, amefuzu kujiunga na chuo kikuu cha Harvard.
Taarifa kutoka ikulu ya White House imesema kuwa Malia ambaye amekuwa mapumzikoni baada ya
kuhitimu masomo ya chuo cha upili, atajiunga na chuo hicho cha kifahari mwakani.
Malia ataendelea na likizo yake kabla ya kujiunga na Harvard mwakani.'' taarifa hiyo ya ikulu ilielezea.
Malia mwenye umri wa miaka 17 atakuwa anafuata nyayo za wazazi wake rais Obama na Mitchel ,ambao wote walihitimu na Shahada ya Sheria kutoka Kitivo cha Sheria cha chuo kikuu cha Harvard.
Chaguo lake la chuo kikuu limekuwa likijadiliwa haswa na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
Malia ndiye binti wa kwanza wa rais Obama.
Binti mwengine wa rais huyo mwenye asili ya Kenya anaitwa Sasha na anaumri wa miaka 15.



Sasha anahudhuria shule ya upili ya kifahari ya Sidwell Friends.
Rais Obama amesema kuwa ataendelea kuishi mjini Washington Marekani hata baada ya kukamilisha kipindi chake cha urais wa Marekani hadi pale Sasha atakapotamatisha masomo yake ya shule ya upili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728