"Hongera Emmanuel Elibariki "Ney wa Mitego" na pia pole zangu za dhati. Bob Marley aliwahi kusema maneno haya "Emancipate yourself from mental slavery none but ourselves can free our mind..." Wasanii wana sehemu kubwa sana ya kubadili fikra za watu, Na muziki ni silaha muhimu kwenye mabadiliko ya fikra na safari ya kujengea watu Uhuru wa kutoa maoni .
Nampongeza Rais kwa kumuelekeza Waziri Mwakyembe kuruhusu Nyimbo ya Ney na mawazo yake. Kuzuia watu kuongea ama kutoa fikra zao hadhari ni hatari kwa jamii yetu.
Ni lazima serikali ijenge daraja la kupitisha kujadili maoni ya watu.
Hiyo ni njia bora ya kujenga Taifa imara.
Muziki ni burudani, muziki ni elimu, muziki ni umoja na muziki ni nyezo inayounganisha jamii. @naytrueboy"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni