MWANAFUNZI wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Changwe wilayani humu, Chiza Daniel (14), mkazi wa Kijiji cha Changwe Wilaya ya Buhigwe mkoani
Kigoma, amefariki dunia papo hapo baada ya kupigwa na radi wakati akifua nguo nyumbani kwao.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Obadiah Nselu, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7:00 mchana kijiji cha Changwe Kata ya Mubanga Tarafa ya Manyovu Wilaya ya Buhingwe.
Kamanda Nselu alisema mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kupigwa na radi kiunoni akiwa anafua nguo zake nje ya nyumba yao.
Alisema mwili wa marehemu ulipelekwa Hospitali ya Mkoa Maweni na kufanyiwa uchunguzi kisha kukabidhiwa ndugu kwa maziko.
Aidha, Kamanda Nselu alisema mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika kesho katika Kijiji cha Changwe.
21 Machi 2017
Mwanafunzi afariki baada ya kupigwa na Radi wakati akifua nguo
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni