Unaweza kutoamini lakini inapofikia wakati ikathibitishwa ni lazima kuamini. Tumekuwa tukiamini kwa kusikia na wakati mwingine kwa kuona kwa macho yetu kuwa Kinyonga ndiye kiumbe Pekee anayeweza kubadilisha rangi yake kulingana na
mazingira.
Leo nimekutana na hii ya Wanasayansi wa Argentina ambao wamemgundua Chura wa kwanza duniani mwenye uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi yake anapopigwa na mwanga wa jua ambapo wanasayansi hao walisema Chura huyo hubadilika kutoka rangi ya Kahawia kwenda rangi ya Kijani iliyofifia au Blue pindi anapokutana na mwanga mkali wa jua.
Wanasayansi hao walisema Chura huyo hukoza rangi zaidi anapokutana na jua kali zaidi na rangi yake huzidi kupungua akipigwa na mwanga mdogo wa jua wakidai ni jambo ambalo hawakulitegemea ukiwa ni ugunduzi mpya kwao kwa kuwa ni mara chache viumbe wa ardhini kuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi zao.
16 Machi 2017
Wanasayansi wagundua kiumbe kingine kinachobadilika rangi kama Kinyong
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni