Toka sakata la Makonda kuvamia,nimejipa muda kuangalia hii Tv,vipindi na nyimbo wanazopiga ni kama wanafikisha ujumbe kwa mkulu na RC wa Dsm.Wanapiga nyimbo za "vijembe" na leo wameimba wimbo wa "Solidality Forever" huku wameshikana mikono studio.
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha "Clouds 360",nimesikiliza nukuu zilizotolewa na watangaji wote watatu, lakini nimefurahia zaidi nukuu ya pili ya mtangazaji Sam Sasali
"Kuanzia sasa nitasoma kila kitu, nitasoma kila gazeti liwe la michezo siasa na kila kitu sitaki kupangiwa, sitaki kupigiwa simu za maelekezo kwamba hiyo story soma au hiyo usisome"
Hii imetoa picha kuwa kumbe hawa jamaa huko nyuma walikuwa "wanatumika",walikuwa wanapangiwa nini cha kusoma na kujadili kwa maslahi ya watu fulani.
Ndio maana katika siku zote za sakata la "Bashite na vyeti feki",hawa Clouds inasemekana hawakulizungumzia sana wala kulijadili kwa mapana ktk vipindi vyao.Lakini toka jana na leo,kuanzia kipindi cha muziki cha XXL mpaka Alasiri ya Clouds Tv,mjadala wa vyeti ulianza kushika hatamu.
Huu ni ujumbe kwa hawa wamiliki wa vyombo vya habari,zama za unafiki zimekwisha,wasimamie ukweli,maana wengine wanashindwa kusimama na Clouds Media Group sbb kwa muda mrefu walikuwa kama tawi la chama na kitengo cha propaganda mpaka wengine "tukazila" kuwafuatilia.Hili ni fundisho kwao.
Source:JamiiForums/Barafu
21 Machi 2017
Watangazaji Clouds Wavunja ukimya wavunja urafiki na Makonda
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni