08 Septemba 2015

Mwanafunzi mwerevu apata alama 0 !


Mwanafunzi aliyepata 0 kwenye mtihani wa mwisho
Maelfu ya wazazi na wanafunzi wamejitokeza kumuunga mkono mwanafunzi mmoja shupavu aliyepata sufuri katika mtihani wake wote wa mwisho.

Amini usiamini,Mariam Malaka ambaye amekuwa mwanafunzi wa kupigiwa mfano nchini Misri kutokana na alama za juu alizopata katika mitihani ya awali, alikuwa na matarajio ya kuzoa alama ya juu zaidi yaani A itakayomwezesha kujiunga na chuo cha mafunzo ya daktari lakini wapi ?
Katika mtihani wake wa mwisho Mariam Malak alipewa alama za chini zaidi .
Hii ikimaanisha kuwa, bi Malak hakuandika hata herufi moja aliyojibu kikamilifu.
Bi Mariam Malak anashuku kuwa kulitokea kosa kubwa kwani yeye alivyofanya mtihani huo hadhani kama angeufeli.
''Kwa kweli sikuamini macho yangu eti nimefeli mtihani wa mwisho'' bi Mariam Malak aliiambia BBC.
Familia yake inadai kuwa huwenda malak ameangushwa mtihani wake wa mwisho maksudi tu kwa sababu ya hila.
Alizimia alipotafuta jina lake na akaikosa katika orodha ya watahiniwa waliopasi mtihani wao wa mwisho.
Malak alikuwa hajaufeli mtihani mmoja bali alikuwa amezoa sufuri katika masomo yote saba.
Yaani alikuwa ameambulia sufuri juu ya mia 0% katika masomo yote saba.
''Hii sio kweli''
Familia yake inadai kuwa huwenda malak ameangushwa mtihani wake wa mwisho maksudi tu kwa sababu ya hila.
Awali ilidhaniwa kuwa alichukiwa kwa sababu yeye ni wa kutoka kwenye tabaka la Wamisri wachache ambao ni wakristo wa kicoptic lakini dhana hio ilikataliwa.
Familia yake inahofia huenda hii ikawa ni njama ya kumpokonya mwanawao ndoto yake ya kuwa daktari.
Familia yake imekutana na waziri mkuu huku ukurasa wa facebook kushinikiza uchunguzi wa kina ufanywe ukiwa na wafuasi elfu 30.000.
Wizara ya Elimu imelazimika kumpa mtihani wa kubaini iwapo hati iliyowakilishwa kwa jina lake ni yake haswa ama ni ghushi, hata hivyo ikatoa uamuzi kuwa ilikuwa yake haswa.
Hata hivyo maelfu ya watu waliotazama nakala za hati aliyoandika kwenye runinga walisema hazifanani kabisa na zile zilizopewa jina lake.
Kufuatia tofauti hiyo, ukurasa ulianzishwa kwa nia ya kuishinikiza wizara ya elimu kuingilia kati kutanzua kitendawaili hicho.
Ukurasa huo unawafuasi takriban 30,000 kufikia sasa.
Tayari watu kadha wamejitokeza kugharamia malipo yake yote ya chuo kikuu.
Ndugu yake Mina anasema kuwa wanashuku majibu yake yalipewa mtu mwengine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728