Jeshi la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini Mashariki la Borno
Jeshi la Nigeria
limepiga marufuku matumizi ya farasi na punda katika jimbo la Kaskazini
Mashariki la Borno, kama sehemu ya juhudi za vita dhidi ya Boko Haram .
Kundi hilo limekua likitumia farasi kutekeleza mashambulizi dhidi ya wanavijiji Jimbo la Borno ndio kitovu cha vuguvugu la Boko Haram
Huku jeshi la Nigeria likionekana kupata mafanikio
katika vita vyake dhidi ya Boko Haram, kundi hilo linaripotiwa
kukabiliwa na kibarua kigumu kupata mafuta ya kuweka kwenye magari yake
kwa hivyo hutumia farasi kwa usafiri mbadala.
Lakini tayari kuna
marufuku ya matumizi ya piki piki ambazo zilikuwa zikitumiwa na
wanamgambo wa Kiislamu wa Boko Haram kuwasafirisha wapiganaji wake
katika mashambulizi. Kufuatia upungufu wa Mafuta Boko Haram imekuwa ikitumia punda na farasi kufanya mashambulizi yake
Pikipiki hizo zilirahisisha kutoroka kwa
washambulizi , kwa hivyo kwa sasa kuna hofu kwamba marufuku ya sasa
itadhoofisha zaidi uchumi wa maeneo ya vijijini na kuathiri maisha ya
watu wa kawaida.
Punda hutumiwa kwa kusafirishia bidhaa na mara nyingi farasi huendeshwa katika tamasha za kidini na kitamaduni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni