Papa Francis
anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki
waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa
katika kanisa hilo .
Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .
Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .
Mwandishi wa BBC mjini Vatican anasema kuwa Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni