Utafiti wa hivi
karibuni uliowachunguza wanafunzi 1000 Korea Kusini umebaini kuwa
asilimia 72 ya watoto wanapata simu wakifikia umri wa miaka 11 au 12.
Aidha kwa Wanafunzi hao huzitumia simu hizo za kisasa kwa karibu saa tano na nusu ya muda wao kwa siku.
Matokeo yake ni kuwa asilimia 25 ya watoto ama mmoja kati ya wanafunzi 4 ametajwa kuwa na uraibu wa simu hizo.
Simu za kisasa za mkononi katika kamataifa ya Asia zimekua kama ibaada.
Kwa mfano, nchini Japan, kuna desturi maalum ya simu za mkononi inayojulikana kama Keitai;Wanatumia simu za mikononi za kisasa kutumiana picha za chakula na vitu mbalimbali.
Lakini utumizi huu wa simu za mkononi kwa kiasi cha kupindukia umewapata baadhi yao katika mazingira yasiyo ya kawaida.
Mtalii mmoja raia wa Taiwan naye nusura atumbukia baharini, kisa na maana , simu.
Yamkini alikuwa akichapisha ujumbe na wenzake kiasi kuwa haoni anakokwenda.
Nomophobia
Nchi ya Singapore karibu kila raia anamiliki simu ya kisasa ya mkononi, raia huko ni milioni sita pekee.
Kwa sababu ya uraibu huu nchi imejenga kiliniki maalum ya kuwashugulikia walio na tatizo la Nomophobia, yaani kuipenda simu kupindukia.
Mmoja anayepitia matibabu ya kuugua kwa kuikosa simu ni kijana wa miaka 19 wa Korea Kusini, Emma Yoon.
Amekua na tatizo hili tangu mwaka wa 2013.
Imekua ni kama mmoja ya viungo vyake.
Wazazi wake wanasema penzi la simu alilonalo mwanao limeathiri maisha yake ikiwemo kushindwa kwenda shuleni wakati mwingine.
Lakini hofu sasa ni kwa watoto wachanga ambao pia nao wamejipata kwenye uraibu huu.
Simu siku hizi bara Asia inatumika kufanya kazi ya ziada miongoni mwa wanafunzi ama ukipenda Homework.
Ndio maana hata China wamefungua kiliniki yao ya kutibu Nomophobia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni