02 Machi 2016

UEFA yaipiga marufuku Galatasaray

Klabu ya Uturuki Galatasaray imepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano yeyote yalioandaliwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA kwa kipindi cha miaka miwili kwa kukiuka kanuni za uadilifu wa kifedha

(financial fair play).
Mabingwa hao wa soka ya Uturuki walisajili hasara kubwa iliyolazimu UEFA kuchukua hatua baada ya ufichuzi mwezi Januari.
Galatasaray ilifuzu kwa hatua ya makundi katika kinyang'anyiro cha kuwania kombe la mabingwa barani Ulaya msimu uliopita.
Vigogo hao wa soka ya Uturuki wanashikilia nafasi ya 5 hivi sasa katika jedwali la ligi kuu.


Galatasaray, ambayo iliilaza Arsenal kupitia mikwaju ya penalti katika fainali za kuwania kombe la UEFA mwaka wa 2010 wamekuwa wakifuzu kwa mechi za kombe la mabingw barani ulaya katika misimu 4 mfululizo.
Msimu huu wanacheza katika ligi ya daraja la pili yaaani Europa ambapo waliambulia kichapo mikononi mwa Lazio.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728