
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na kura ya kutokuwa na
imani naye bungeni leo, ikiwa ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi
mwaka mmoja. Kura hiyo ya kutokuwa na imani na rais Zuma imeitishwa na
chama cha upinzani cha Democratic Alliance DA.Pia chama hicho
kinajaribu kwa njia ya kisheria kurudisha tena mashtaka ya rushwa dhidi
ya kiongozi huyo, baada ya kutumia kitita kikubwa cha fedha kukarabati
makaazi yake ya binafsi kijijini anakotoka. Zaidi sikiliza matangazo
yetu ya leo Jioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni