14:00 Wawafahamu wagombea wote wa urais walio kwenye karatasi za kura visiwani Zanzibar? Kuna wagombea 14. Majina yao ndiyo haya:
1
Khamis Iddi Lila
ACT-W
2
Juma Ali Khatib
ADA-TADEA
3
Hamad Rashid Mohamed
ADC
4
Said Soud Said
AFP
5
Ali Khatib Ali
CCK
6
Ali Mohamed Shein
CCM
7
Mohammed Massoud Rashid
CHAUMMA
8
Seif Sharif Hamad
CUF
9
Taibu Mussa Juma
DM
10
Abdalla Kombo Khamis
DP
11
Kassim Bakar Aly
JAHAZI
12
Seif Ali Iddi
NRA
13
Issa Mohammed Zonga
SAU
14
Hafidh Hassan Suleiman
TLP
13:00 Mji Mkongwe (Stone Town)
ambao ni maarufu sana kwa watalii hauna watu wengi. Mwandishi wa BBC
Tulanana Bohela amepiga picha hizi zinazoonesha mtaa huo ukiwa kama
mahame. 11:15 Mwandishi wa BBC Halima
Nyanza aliyeko Zanzibar anasema idadi ya watu waliojitokeza katika
baadhi ya vituo ni ndogo, tofauti na uchaguzi wa awali Oktoba 25, mwaka
jana. Baadhi ya mitaa imeonekana kutulia huku ulinzi ukiwa umeimarishwa
katika baadhi ya maeneo. 10:30 Mgombea
urais wa chama cha ADC Hamad Rashid amepiga kura yake kituo cha
Tondooni Wawi wilaya ya Chake-Chake, mkoa wa Kusini Pemba. Amesema:
"Nina imani ya kuwa Rais, nikikosa nitakuwa Makamu wa Rais". 10:00 Mwanamke akitumbukiza kura kwenye kijisanduku kituo cha Kiembe, Samaki. Upigaji kura unaendelea. 08:50 Mgombea urais wa Chama cha
Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein amezungumza na
wanahabari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera
kisiwani Unguja.
Mwanzo amezungumzia hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi huo.
Kuhusu amani na utulivu, amesema anaamini kutakuwa na utulivu visiwani.
Hii hapa video yake akizungumza:
08:00 Maafisa wa usalama wakishika doria mjini Chake kisiwani Pemba. 07:50 Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa.
Hapa
chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa
na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi
unaoendelea Zanzibar. Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu
waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka
Ulaya ambao hawakuwa na habari. 07:44 Usalama umeimarishwa
visiwani. Hapa chini ni maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa
kabla ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Unguja. 07:42 Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba. 07:30 Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba. Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi. 07:20 Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein, mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura Unguja. 07:05 Mgombea wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein amepiga kura yake katika kituo cha Bungi, Kibera katika kisiwa cha Unguja. Image caption
Dkt Shein akioneasha wino kwenye kidole chake
07:00 Vituo vingi vya kupigia kura vimefunguliwa. 06:50 Maafisa wa uchaguzi wanajiandaa kufungua vituo. Vituo vinafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi alasiri. 06:40 Wapiga kura kituo cha Bungi, Unguja wasubiri kituo kifunguliwe. 06:35 Katika vituo vingi, wapiga
kura hajawafika. Lakini maafisa wa tume tayari wamo vituoni pamoja na
maafisa wa usalama. Hata ni kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba. 06:30 Hujambo! Wapiga kura visiwani
Zanzibar wanashiriki uchaguzi wa marudio leo baada ya matokeo ya
uchaguzi uliofanyika 25 Oktoba mwaka jana kufutwa na tume ya uchaguzi.
Chama cha CUF kinasusia uchaguzi huo.
Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu uchaguzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni