01 Machi 2016

Wanaoishi katika mapipa ya taka UK waongezeka


Idadi ya watu wasio na makao na ambao sasa wanaishi katika mapipa ya taka inaendelea kuongezeka nchini Uingereza kulingana na kampuni kubwa ya kuzoa takataka nchini humo.
Lakini ni kwa nini hili linatokea?
''Katika barabara unatukanwa na hata kunyanyaswa.Usiku uliopita vijana wachache walikuwa wanatembea karibu yangu na mwengine akanipiga teke la uso.Lakini katika mapipa unaweza kujificha ili watu wasikuone.Kuna joto hakuna mtu anayejua ulipo,''George analezea kuhusu barabara ya Bristol.
Amekuwa bila makao tangu alipopoteza kazi yake ya uhandisi kabla ya krisimasi,na kumfanya kushindwa kulipa kodi ya nyumba.


George ni miongoni mwa idadi kubwa ya raia nchini Uingereza aliyepatikana akilala katika mapipa ya takata kulingana na kampuni hiyo ya kuzoa taka ya Biffa.
Mnamo mwaka 2014 kampuni hiyo iligundua watu 31 waliokuwa wakilala katika mapipa tofauti ya takataka.
Mwaka mmoja baadaye idadi hiyo iliongezeka na kufikia 93 na mwaka huu ambao unaisha mwezi Machi, idadi hiyo imefikia 175 kufikia sasa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728