07 Machi 2016

Ubishi wa Messi na Ronaldo wasababisha mauti

 
Polisi nchini India wamemfungulia mashtaka ya mauaji mtu mmoja aliyemdunga kisu rafikiye
waliyekosana kuhusu nani kati ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.
Raia huyo wa Nigeria alimdunga kisu mwezake vilevile mnigeria ambaye walikuwa wakibishana naye.
Inspekta mkuu wa polisi Kiran Kabadi ameiambia shirika la habari la AFP kuwa Michael Chukwuma, 21 ameshtakiwa kwa kuua katika mji wa Mumbai.
Yamkini yeye na mwenzake walianza gumzo kuhusu mchezaji bora katika kitongoji kimoja cha Nallasopara.
Chukwuma na wenzake walikuwa wamemtembelea marehemu kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

''Mmoja wao alikuwa ni shabiki sugu wa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Messi huku marehemu akimshabikia mfungaji mabao wa Ureno na Real Madrid Ronaldo''.
''Na kwa sababu ambayo haijulikani Chukwuma alimdunga marehemu mwenye umri wa miaka 34 kwa kisu na kumuua papo hapo.'' alisema Inspekta hyo wa Polisi.
Walioshuhudia wanasema kuwa marehemu alimrushia mshukiwa glasi usoni na mshukiwa akamshinda nguvu na kumdunga na ile glasi iliyovunjika, aliongezea Kabadi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728