25 Machi 2016

Hakuna dalili ya kupatikana suluhu ya kudumu Syria

Wakati mazungumzo ya amani ya Syria yakiakhirishwa baada ya kufanyika kwa siku 10, bado hakuna dalili yoyote ya kupatikana suluhu ya kudumu katika mzozo huo.
Genf Friedensverhandlungen zu Krieg in Syrien - Staffan de Mistura mit Bashar al Jaafari Mjumbe wa serikali katika mazungumzo ya Syria Bashar al Jafari na mjumbe wa UN Staffan de Mistura

Mpango wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwaajili ya Syria Staffan de Mistura ni kuwepo kipindi cha mpito wa kisiasa nchini Syria.
Licha ya kwamba de Mistura alifanikiwa kudhibiti mazungumzo hayo kati ya wajumbe wa serikali na wale wa upinzani, hakuweza kufanikiwa zaidi kuziweka pande hizo zinazohasimiana katika meza moja ya mazungumzo au kujadili ajenda ya baraza la usalama la umoja wa mataifa la kutaka uwepo wa kipindi cha mpito wa kisiasa.
Aidha de Mistura amesema kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa na wanamgambo wa dola la kiislamu nchini ubelgiji na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 30, inaonesha kuwa njia moja ya kuushinda ugaidi ni kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
Schweiz Syrien-Friedensgespräche in Genf Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwaajili ya Syria Staffan de Mistura
Baada ya mapigano nchini humo kuingia mwaka wake wa tano na kila upande katika mzozo huo ukishindwa kuwadhibiti wenzao kijeshi, pande hizo zinazohasimiana zimeamua kuwa hakuna njia nyengine ya kusuluhisha mgogoro isipokuwa mazungumzo.
Hata hivyo Urusi na Marekani wanaounga mkono mazungmzo hayo wanashirikiana pamoja kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha zaidi ya watu 250,000 kuuwawa huku wengine wengi wakiachwa bila makaazi.
Wanamgambo wa IS washambuliwa katika mji wa kale wa Palmyra
Mazungumzo hayo yaliahirishwa siku ya alhamisi huku mjumbe Staffan De Mistura akitangaza tarehe 9 mwezi Aprili kuwa siku ya kuanza tena mazungumzo hayo. Mjumbe wa upande wa serikali ya Syria katika mazungumzo hayo Bashar Ja'afari, alikutana na de Mistura hapo jana lakini hakuweka wazi kila walichokizungumzia.
Kwa upande wake George Sabra mwanachama mkuu katika akamati kuu ya upinzani amesema upande wake uko tayari kuendelea na mazungumzo. " Kupiga hatua katika mazungumzo haya ni ngumu lakini tutaendelea na juhudi za kutafuta muafaka," alisema George Sabra.
Syrien Kampf gegen IS Mashambulio mjini Palmyra
Lakini wachambuizi wanasema iwapo rais Assad hataondoka madarakani kuna wasiwasi wa upinzani kujiondoa katika mazungumzo hayo mjini Geneva.
Huku hayo ya kiarifiwa ndani ya Syria kwenyewe vikosi vya serikali vimeingia katika mji wa kale wa Palmyra huku vikosi vya Iraq vikitekeleza mashambulizi mjini Mosul dhidi ya wanamgambo wa dola la kiislamu IS. Vikosi hivyo vcya Syria pia vinasaidiwa na vikosi vya kijeshi vya urusi kukabiliana na wanamgambo hao.
Kulingana na wizara ya Ulinzi ya Urusi, ndege zake za kivita zimefanya mashambulizi ya angani 146 katika maeneo ya wanamgambo hao kati ya jumapili na jumatano na kuwauwa magaidi 320.
Mwandishi: Amina Abubakar/AFP/AP
Mhariri: Yusuf Saumu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728