20 Machi 2016

Utata kuhusu mwandishi wa DW Zanzibar

SalmaSiku mbili zimepita tangu kutoweka kwa mwakilishi wa kituo cha redio cha Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle) Salma Said visiwani Zanzibar na hadi sasa hajulikani alipo.
Taasisi za kiraia, mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na jumuiya ya waandishi wa habari nchini Tanzania wamelaani kutekwa nyara kwa mwandishi huyo.
Mashirika mengine yameitaka serikali kuhakikisha kwamba Salma Said, mwenye umri wa miaka 45, anapatikana akiwa salama.

Sauti ya Ujerumani ilitangaza Ijumaa kwamba mwandishi huyo alikuwa ametekwa na watu wasiojulikana.
“Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kuwa mwakilishi wetu visiwani Zanzibar, Salma Said (pichani), amekamatwa na watu wasiofahamika kwa sababu ambazo bado DW haijazielewa. Tumezungumza naye akiwa sehemu anayosemekana kushikiliwa na sikiliza kwenye matangazo yetu ya jioni,” idhaa hiyo iliandika katika Facebook.
Mume wa Salma Said, Bw Ali Salim Khamis, amezungumza na mwandishi wa BBC Halima Nyanza kuhusu alivyoachana na mkewe uwanja wa ndege kabla ya kutoweka.
“Yeye alikuwa anaenda Dar es Salaam kwa ajili ya ‘check-in’ na mimi ndiye niliyempeleka uwanja wa ndege mpaka ‘amecheck-in’ pale ndani mi ndio nikaondoka uwanja wa ndege,” amesema Bw Khamis.
“Baada ya muda akaniambia ndege yao imechelewa, itachelewa kuondoka lakini haikupita muda mrefu akanijulisha kwamba kwa njia ya SMS kwamba saa hivi niko chini ya ulinzi nishakamatwa hapa.”
Bw Edwin Nsoko ambaye ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari wanaopinga matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania amesema wamekuwa wakiwasiliana na vyombo vya usalama na wadau kuhakikisha Bi Salma “anarejeshwa na anakuwa salama na kuendelea na majukumu yake kama kawaida”.
Amesema kufikia sasa hawajaridhishwa na taarifa kutoka kwa vikosi vya usalama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728