Ukuaji huo hatahivyo umekuwa na athari kubwa za ajali za barabarni huku data iliotolewa na
kamanda wa idara ya trafiki nchini Tanzania Mohammed Mpinga ikionyesha kuwa ajali zinazohusishwa na pikipiki ambazo hutumika kwa uchukuzi hushirikisha asilimia 60 ya jumla ya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali kuu ya Muhimbili.
Nchini Tanzania ajali za barabarani ziliwaua takriban watu 3,468 mwaka 2015,ambapo ajali zinazohusisha pikipiki ziko katika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo nchini humo baada ya HIV na Malaria.
Mpinga hatahivyo amesema kuwa pikipiki zitaimarisha viwango vya usalama barabarani kupitia kuvaa kofia za helmet,kutobeba zaidi ya mteja mmoja mbali na kutokunywa pombe wakati mtu anapoendesha.
Vilevile amewaonya wale wanaohusika katika uhalifu akisisitiza usajili wa pikipiki kote nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni