02 Machi 2016

Mitumba kupigwa marufuku Afrika Mashariki


NguoViongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki waliokutana leo mjini Arusha, Tanzania wameamua kupiga marufuku uagizaji wa nguo za viatu kuu vya mitumba.
Utekelezaji wake utakuwa baada ya miaka mitatu.
Marufuku hiyo ni moja ya hatua zilizopendekezwa ilikuinua viwanda vya nguo katika kanda ya Afrika Mashariki.

Serikali za Afrika Mashariki zimekuwa zikilaumu uagizaji wa nguo na viatu vilivyotumika kama moja ya sababu zinazofanya viwanda vya nguo na ngozi kusambaratika na hivyo kuwanyima wenyeji nafasi ya ajira.


Nguo hizo hutegemewa sana na watu wenye mapato ya chini kutokana na bei yake nafuu.
Kadhalika, wauzaji wa nguo hizo wasafirishaji,waagizaji wote huzitegemea kupata mkate wao wa kila siku hii ikichangia pato la nchi na ajira kwa maelfu ya watu ambao huhudumu katika biashara hiyo.
Viongozi hao pia watajadili pendekezo la kupunguza kiasi cha magari yaliyotumika yanayoingizwa kanda hii.
Lengo lao likiwa kutafuta mbinu ya kusaidia viwanda vya utengenezaji magari vinavyoendesha biashara Afrika Mashariki.
Marais Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni (Uganda) walihudhuria mkutano huo mjini Arusha.

aombi ya Sudan Kusini na Somalia kutaka kujiunga na jumuiya hiyo pia yalijadiliwa. Sudan Kusini ilikubaliwa kujiunga kama mwanachama wa 6 wa muungano wa mataifa ya Afrika Mashariki.
Wakati wa mkutano huo, viongozi hao wanatarajiwa kuzindua pasipoti ya pamoja ya Afrika Mashariki ambayo itakuwa katika mfumo wa elektroniki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU
KUWEKA TANGAZO LAKO HAPA NI BEI NAFUU

TANGAZO LA KAZI -Commited youth agricultural organisation CYAO is looking for a person who is specialised in agriculture

POSITION DESRIPTION;

Agricultural Technician

Qualifications

Diploma in agriculture

Mode of application applicant must send an updated Cv,birth cirtificate,one recent passport size, an accademic cirtificate, age limit 20 to 35

apply to Project cordinator,Commited youth agriculture organisation,P.O.Box 78438 Dar es salaam or you can call through +255657990920/+255754823728